Gladys Chania, mke wa George Mwangi, kwa sasa yuko kizuizini kuhusiana na mauaji ya mumewe. |
KUTOKA NCHINI KENYA
Familia yake waliokuwepo wakati wa zoezi hilo walieleza kuwa majeraha kwenye mwili wake yalionyesha alikumbana na kifo chake kwa njia ya kutisha.
Zaidi ya hayo, marehemu pia alikuwa na majeraha kwenye vidole vyake, kuashiria kuwa mfanyabiashara huyo huenda alipigania maisha yake wakati wa mateso.
Hasa, vidole vya mkono wake wa kushoto ndivyo vilivyoathiriwa zaidi.
Uchunguzi wa maiti ulifanyika mnamo Oktoba 21 katika hospitali moja ya jiji hata wakati wapelelezi wakiendersha uchunguzi wao kuhusu mauaji hayo.
Asema Haoni Haya Kuwa Nazo Familia yake inaamini kuwa matokeo ya uchunguzi wa maiti yatasaidia maafisa katika kutegua kesi hiyo.
Familia yake bado haijapanga tarehe ya kuzikwa kwkake huku pande mbili zinazozozana zikipigania kupewa kibali cha kumzika.
Wakati uo huo, mkewe, mwanasiasa wa Kiambu, alisalia rumande kama mshukiwa mkuu wa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), marehemu aliuawa nyumbani kwake Mang’u kabla ya mwili wake kutupwa katika msitu jirani.
“Vipande vya chuma vikiwa na damu, shuka, mapazia na nguo zilizokuwa na damu zilikuwa sehemu ya ushahidi vilivyopatikana ndani ya nyumba hiyo na makachero kutoka Maabara ya Kitaifa ya Uchunguzi wa Kitaifa ya DCI. "Wapelelezi kutoka Ofisi ya Utafiti wa Uhalifu na Ujasusi, Idara ya Mauaji, Eneo la Uhalifu wa Kisheria na vitengo vya Picha wamehitimisha kuwa aliuawa katika chumba chake cha kulala kwenye ghorofa ya juu," DCI ilisema wakati huo.
Mauaji ya mfanyabiashara huyo yalihusishwa na mapenzi kwani polisi walisema kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa na mmpango wake wa kando ambaye alihudhuria hafla za familia naye siku chache kabla ya kifo chake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.