ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 27, 2022

RUTO AHATARISHA KUWEKEWA VIKWAZO NA MAREKANI KWA KUTANGAZA YUKO RADHI KUNUNUA MAFUTA URUSI.

Rais Ruto.

Rais William Ruto yuko huru kufanya biashara ya Urusi ambayo imetengwa kimataifa, baada ya kuivamia kivita taifa la Ukraine mnamo Februari 24, 2022. 

 Kwenye mahojiano na kituo cha BBC, Rais Ruto alisema yuko radhi kununua mafuta kutoka Urusi, ikiwa ndio mojawapo ya njia mbadadala kwa Kenya kuipata kwa bei nafuu.

 Ruto alisema kwamba anaangalia kila mbinu itakayowezesha gharama ya mafuta kushuka humu nchini, baada ya kuondoa ruzuku iliyosababisha bidhaa hiyo kuuzwa kwa bei ghali katika historia ya Kenya. 

Rais Putin.

"Sasa ajenda yangu ni kuhakikisha uhusiano wa serikali kwa serikali, ambao utahakikisha kuteremka kwa bei ya mafuta," Rais Ruto alisema.

Alipoulizwa iwapo anaweza kuyanunua mafuta hayo kutoka Urusi, Ruto alijibu; "Mbinu zote zilizopo kwetu zitatumika kama taifa."

 Tangazo la Ruto kuwa serikali yake iko radhi kufanya biashara na nchi ya Urusi bila shaka huenda ikamuweka katika njia panda na mataifa ya magharibi, ambayo yameiwekea vikwazo serikali ya Vladimir Putin. Mapema mwezi huu, Marekani ilitishia kuwawekea vikwazo wanunuzi wa mafuta ya Urusi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.