ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 19, 2022

KESI YA ZUMARIDI YAAHIRISHWA BAADA YA MSHTAKIWA MWENZA KUDONDOKA MAHAKAMANI.

Mwanza, September 19.2022

Kesi namba  12 ya mwaka 2022 inayomkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wenzake 84 ya kufanya mkusanyiko usio halili  imeshindwa kuendelea kusikilizwa baada ya mshtakiwa namba 38 Maria Julius  kuaguka ghafla mahakamani  hapo.

Kesi hiyo imeshindwa kuendelea kusikilizwa Mbele ya hakimu mkazi Mkoa wa Mwanza Clesencia Mushi baada ya mshtakiwa huyo aliyejulikana kwa jina Maria Julius namba 38 kuugua ghafla na kudondokana mahakamani hapo.

Wakili wa utetezi katika kesi hiyo  
ambao umeongozwa na Amri Linus ameiomba mahakama hiyo kutoendelea na kesi hiyo leo kutokana na mteja wao Maria Julius kuugua ghafla na kudondoka akiwa  mahakamani  hapo hivyo ameiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine ya kesi hiyo wakati mteja wake akipelekwa hospitali kwaajili ya kupata matibabu.

Kutokana na hoja hiyo upande wa jamuhuri ambao umeongozwa na wakili Dorcas Akyoo akakubali maombi hayo yaliyowasilishwa na upande wa utetezi.

Kwa upande wake hakimu mkazi Mkoa wa Mwanza Clesencia Mushi baada ya kusiliza pande zote mbili ameiahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa tena.

Zumaridi amerudishwa rumade huku washtakiwa wengine wakiwa nje kwa dhamana.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo wakili upande wa utetezi Erick Mutta ameeleza mwenendo wa kesi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.