ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 12, 2022

Raphael Tuju Asifia Matokeo ya Raila Mlima Kenya "Yuko Tayari Kumrithi Uhuru"


Afisa Mkuu Mtendaji wa Azimio La Umoja, Raphael Tuju amesema kuwa muungano huo ulifurahishwa na matokeo ya kura ya Raila Odinga katika eneo la Mlima Kenya. 

Tuju alishikilia kuwa Raila na mgombea mwenza wake, Martha Karua, walifanya vyema sana katika eneo linalotawaliwa na United Democratic Alliance (UDA).

 Alieleza kuwa matokeo hayo yalionyesha kuwa Raila bado ana uzito katika eneo hilo licha ya muungano wa Kenya Kwanza unaohusishwa na Naibu Rais William Ruto kujinyakulia kura nyingi. 

Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Chama cha Jubilee alionyesha imani kuwa kutokana na matokeo hayo Raila yuko tayari kumrithi Rais Uhuru Kenyatta. 

"Tuna matokeo ya wale waliompigia kura Raila, bora zaidi kuliko ilivyokuwa miezi sita iliyopita au mwaka mmoja uliopita.La muhimu ni kwamba amefanya vyema sana, na tunatarajia habari njema na jukumu langu hapa Bomas kuhakikisha kila kitu kinaendelea vyema," Tuju aliongeza. 

Tuju pia alipongeza vyombo vya habari kwa kuonyesha matokeo tofauti, akibainisha kuwa inasaidia kuweka chombo cha uchaguzi kinachoongozwa na Wafula Chebukati kudhibiti. "Nadhani ni maendeleo chanya kwamba vyombo vya habari vilishiriki katika mchakato huu wa kisiasa wa uchaguzi. Lakini tunapaswa kufahamu kwamba kuna vikwazo," Tuju aliongeza. 

Ruto avuna zaidi Maoni yake yanakujia baada ya matokeo yaliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuashiria kuwa kiongozi wa Chama cha Narc Kenya Martha Karua alifedheheshwa nyumbani kwake kaunti ya Kirinyaga baada ya chama cha United Democratic Alliance (UDA), unaoongozwa na mgombea urais wa Kenya Kwanza William Ruto kunyakua viti vyote vya ubunge.

Vyama vinavyohusishwa na muungano wa Azimio ya Raila Odinga, ambao una Martha Karua kama mgombea mwenza, umeshindwa kunyakua kiti hata kimoja cha ubunge Kirinyaga. Daily Nation linaripoti kwamba wagombeaji wa UDA katika Kirinyaga ya Kati, Gichugu, Ndia na Mwea walishinda viti vyao mtawalia, na kuipa Narc Kenya na vyama vingine vya Azimio fedheha. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.