Barasa alijipeleka katika kituo cha polisi cha Bungoma Ijumaa Agosti 12 asubuhi kuhusiana na kisa cha mauaji.
Alhamisi Agosti 11 polisi walitoa makataa ya saa sita kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi. Mkurugenzi wa DCI Georhge Kinoti alisema Barasa atahojiwa kuhusiana na kifo cha msaidizi wa mpinzani wake Brian Olunga.
Kinoti alikuwa ametoa onyo pia kwa yeyote ambaye anamficha Barasa aksiema kuwa atachukuliwa hatua madhubuti.
"Hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote ambaye atapatikana amekuwa akimficha mshukiwa huyo wa mauaji," Kinoti alisema Aidha kikosi maalum kilikuwa kimeundwa kumsaka Barasa tangu aingia mafichoni baada ya kuripotiwa kumpiga risasi Olunga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.