Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kudaiwa kumuua mlinzi wa mpinzani wake kwa kumpiga risasi kichwani mnamo Jumanne, Agosti 9.
Mbunge huyo ambaye ni mshukiwa mkuu katika mauaji ya Brian Olunga ambaye alikuwa mlinzi wa mpinzani wake mkuu Brian Khaemba, alizungumza kupitia kwa mtandao wa kijamii baada ya kutangazwa mshindi wa ubunge wa Kimilili.
Barasa ambaye aligombea kwa tiketi ya chama cha UDA alifanikiwa kutetea kiti chake kwa kura 26,861 dhidi ya kura 9,497 za Khaemba wa DAP-K na kuwashukuru wakaazi wa Kimilili kwa kumpa muhula mwingine wa kuwahudumia kama mbunge wao.
“Asante sana watu wa eneo bunge la Kimilili kwa kunichagua kwa kura nyingi sana kwa muhula mwingine. Nawapenda sana,” Barasa aliandika kwenye mitandao ya Facebook na Twitter.
Barasa atuhumiwa kumuua mlinzi wa mpinzani wake Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, Barasa alimpiga risasi kichwani msaidizi wa mpinzani wake Brian Khaemba katika kituo cha kupigia kura cha Chebukwabi.
Kisa hicho kilitokea majira ya saa kumi na mbili jioni, Barasa na Khaemba walipokutana katika kituo hicho kuangalia zoezi la kuhesabu kura.
“Didmus Barasa alichomoa bastola yake na kumlenga msaidizi wa Khaemba kwa jina Brian Olunga. Alimpiga risasi upande wa mbele wa kichwa alikobubujika damu nyingi,” taarifa ya polisi inasema.
Polisi washuku Barasa alitorokea Uganda
Polisi wanashuku kuwa mbunge huyo huenda alitorokea taifa jirani la Uganda ambako anaendelea kujificha huku msako dhidi yake ukiendelea.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.