Na Oscar Assenga,TANGA.
ASKOFU na Mwenyekiti wa kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Dogo la Kaskazini Mashariki mwa Tanzania Mussa Nzumbi amesema suala la Sensa ya Watu na Makazi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi huku akieleza maana hata bibilia inasema wana wa Israel walihesabiwa
Huku akiwahimiza waumini wa kanisa hilo kuhakikisha wanashiriki kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kikamilifu ili Taifa liweza kujiua idadi ya watu na kuweza kupanga mipango ya kuweza kuwahudumia.
Nzumbi aliyasema hayo wakati wa vikao vya maandalizi ya Jubilee ya miaka 50 ya Kanisa hilo katika kanda ya Tanga ambapo alisema wakati wanaelekea kwenye maadhimisho hayo
Alisema sambamba na hilo wataendelea kuliombea Taifa na viongozi ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuwepo ili wananchi waweze kupata nafasi ya kumuabudu Mungu.
Alisema kuelekea Jubilee hiyo wanamshukuru Mungu amewasaidia kwenye eneo hilo wamekuwa na ongezako kubwa la waumini na huduma za kijamii ikiwemo shule ya Kana Central English Medium na wamekuwa na huduma za kijamii wanazofanya maeneo mbalimbali kama kutoa damu hivyo yote yanawaleta pamoja kutafaraka.
Aidha alisema wanaendelea kuhimiza suala la sensa ya watu na makazi kwa maana suala hilo ni la kibibilia hata wana wa Israel walihisabiwa hivyo ni muhimu kwa sababu ili taifa liweza kujua idadi na serikali iweze kuwahudumia.
“Kwenye Jubilee hii tunaiombea Serikali,wananchi Mungu aendelee kutulinda amani na upendo vikatawale kwenye Taifa letu tunaamini kunapokuwa na utulivu ndio tunapata nafasi ya kwenda kumuambudu mungu kwa uhuru na utulivu zaidi”Alisema Askofu Nzumbi
Hata hivyo alisema kwamba wanaiombea pia Rais ,Serikali ,Mkoa wa Tanga na maeneo mbalimbali yaweze kuwa salama na amani iweze kutawala .
“Tupo hapa Kanda ya Central kwa ajili ya mikutano ya Jubilee ya miaka 50 ya Kanisa hilo Jijini Tanga tunamshukuru Mungu ametusaidia kazi kwenye eneo hilo tumekuwa na ongezako kubwa la waumini na huduma za kijamii kama shule ya Kana Central English Medium na wamekuwa na huduma za kijamii tulizofanya maeneo mbalimbali kama kutoa damu yote hayo yanawaleta pamoja kutafarakani”Alisema
Akofu Nzumbi alisema wana mshukuru Mungu kwa kazi kubwa na Jubilee hiyo inawasaidia wa waumini watafakari mahali walipotoka na mahali wanapokwenda.
“Lakini tuna mikakati kufungua shule ya sekondari Ngomeni itakayosaidia vijana wetu waweze kupata elimu ya dunia sambamba na kufungua kituo vya afya kwenye baadhi ya maeneneo nitoe wito kwa Jamii,kanisa na wananchi tuendelee kushiriki kwa mshikamano tufanye kazi tuendelea kusaidiana”Alisema Askofu Nzumbi
Naye kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Wasabato Julius Mbwambo alisema tukio la kusheherekea maiaka zaidi ya 50 katika kanda ya Tanga ni kazi ya mungu imekuwa sana na kwa miaka hiyo wanakiri kumuona mungu akitembea nao.
Alisema wanaendelea kusherehekea miaka ya kazi ya Mungu na wanaamini yule Mungu aliyekuwepo hapo awali waendelea kuwa naye huku akieleza wataendelea kuifanya kazi ya Mungu mpaka atakaporudi kwa mara ya pili
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.