ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 11, 2022

MSICHANA ANG’ATWA SIKIO NA BABA WA KAMBO AKIMNUSURU MAMA YAKE KATIKA KIPIGO


CHANZOKonzi La Moyo TV Show

Msichana wa Miaka 25 Mkazi wa Buswelu Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza (jina tunalihifadhi) amejikuta akipoteza sikio Katika harakati za kumnusuru Mama yake mzazi aliyekuwa akipigwa na Baba yake wa Kambo. 

Hayo yametokea tarehe 09.07.2022 Siku ya Jumamosi saa Saba usiku  ambapo mwanaume huyo (jina tunalihifadhi) alisadikika kumpiga Mkewe ambaye amejifungua kwa upasuaji Siku sio nyingi kisa kikiwa wivu wa mapenzi.


Msichana huyo akiongea na Konzi la Moyo amesema Katika kuamua ugomvi huo alivamiwa na Baba huyo na kung’atwa siko lake la kulia huku akimtuhumu kuingilia mambo yasiyomhusu. 

Mwanaume huyo amefikishwa kituo cha polisi Kirumba kwa hatua za kisheria. Konzi la Moyo TV Show tutaendelea kukuletea mwendelezo wa taarifa hii. Unaweza ukatoa taarifa ya ukatili kwa namba 116 au piga namba 0736975666 uzungumze na Wataalamu wa elimu nafsi kwa msaada wa UShauri BURE.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.