Makada wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu na Godbless Lema wamesema wanarudi nchini Tanzania muda wowote kuanzia sasa na kwamba hawarudi kukaa tu bali kufanya kazi ya Siasa.
Viongozi hao wa CHADEMA wamesema hayo wakati wakizungumza kwa njia ya mtandao na wanachama wa chama hicho mkoani Tanga.
Makada hao ambao pia ni viongozi wa ngazi za juu kabisa kwenye chama hicho wamesema hayo wakati wakizungumza na mamia ya wananchi na wanachama wa chama hicho kwenye Kongamano la 3 la vuguvugu la kudai Katiba mpya lililofanyika Jijini Tanga.
Awali akizungumza moja kwa moja kwa njia ya mtandao kutoka nchini Ubeljiji, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu amesema kwamba iwapo patafanyika masuala ya kiufunguzi na kiusalama basi atarejea nchini.
” Tunarudi wakati wowote kuanzia sasa, mimi tayari nimeshagawa hadi nguo za baridi japo huku Canada kwasasa hivi Baridi imepungua sana, jana (juzi) tulikuwa tunapanga na mwenzangu ni lini tuanze safari yakurudi nyumbani kwahiyo makamanda msiwe na wasiwasi tunakuja kuongeza nguvu za mapambano ya Katiba Mpya na Demokrasia kwa ujumla” Alisisitiza Lema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.