Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akitoa masaa 48 kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuhakikisha wanamlipa fedha zake mkandarasi wa mradi wa Neghabihi na Ikengeza unaotekelezwa kwa fedha za UVIKO19 wenye jumla ya gharama ya kiasi cha shilingi 643,792097,00.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ya matanki ya maji ambalo limejengwa katika kijiji cha Neghabihi kwa ajili ya kupeleka huduma ya maji kwa wananchi
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa na Mwenyekiti wa Halamshauri ya wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa wakilizisha kuanza kutoka kwa maji ambayo inaashiria kuwa mkandarasi anafanya kazi yake inavyotakiwa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametoa masaa 48 kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuhakikisha wanamlipa fedha zake mkandarasi wa mradi wa Neghabihi na Ikengeza unaotekelezwa kwa fedha za UVIKO19 wenye jumla ya gharama ya kiasi cha shilingi 643,792097,00.
Akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji wilaya ya a Iringa, mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa kazi iliyofanywa na mkandarasi M/S GNMS Contractors kwa kiasi kikubwa imekamilika na kilichobakia ni mkandarasi kulipwa fedha zake.
Moyo alisema kuwa haiwezekani mkandarasi amemaliza kazi lakini mhasibu anachelewesha malipo hivyo alitoa maagizo kwa meneja wa RUWASA wilaya ya Iringa kumlipa fedha mkandarasi huyo.
Alimwagiza meneja amwambie mhasibu amlipe mkandarasi ndani ya masaa 48 kinyume cha hapo atamchukulia hatua za kisheria kwa kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa imeridhishwa na kazi iliyofanywa na mkandarasi huyo.
Moyo alisema kuwa mradi umefika asilimia 73 na hakuna malipo yoyote yale yaliyofanyika hivyo RUWASA wanapaswa kulipa haraka malipo ambayo mkandarasi anadai ili kumalizia kazi iliyobaki ili kufanikisha kuwatua ndoo wanawake.
Kwa upande wake meneja wa RUWASA wilaya ya Iringa Eng Masoud Samila alisema kuwa Mradi huyo ni wa teknolojia ya msukumo kwa kutumia pampu ya umeme ambapo chanzo cha maji ni visima virefu kwa maeneo yote mawili ya Neghabihi na ikengeza.
Eng Samila alisema kuwa Lengo ni kuwapatia wananchi wa eneo husika maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 pamoja kupungunza mlipuko wa magonjwa mbalimbali yanayoweza kujitokeze kutokana na changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama.
Alisema kuwa mradi huo unarajiwa kuwanufaisha wananchi 4920 ambao walikuwa wanakosa maji safi na salama karibu nao hivyo kukamilika kwa mradi huo kutachochea kuongezeka shughuli za kiuchumi kwa wananchi waliopo maeneo ya mradi.
Eng Samila alimalizia kwa kusema kuwa wameyapokea maagizo yote ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa na watayafanyia kazi haraka mno likiwepo swala la kumlipa mkandarasi fedha anazozidia kwa wakati kama walivyoagizwa na mkuu wa wilaya ya Iringa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.