
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kufungua Maonesho ya Saba ya wiki ya Utafiti na Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam, Naibu Makamu Mkuu wa wa Chuo (Utafiti) UDSM, Profesa Bernadetha Killian amewaalika watu wote kuweza kuhudhuria maonesho hayo ya siku mbili ambayo yatakuwa ya kipekee kwa mwaka huu.
Maonesho ya Saba ya Wiki Ya Utafiti na Ubunifu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam yatakayofanyika rasmi Tarehe 24 hadi 26 Mei 2022, Katika Maktaba Mpya Ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.