ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 5, 2022

MNIGERIA ASIYEAMINI KUNA MUNGU AFUNGWA JELA KWA KUKUFURU UISLAMU.

 


Raia wa Nigeria asiyeamini kuna Mungu amehukumiwa kifungo cha miaka 24 jela na mahakama kuu katika jimbo la kaskazini la Kano baada ya kupatikana na hatia ya kukufuru Uislamu.


Mubarak Bala, rais wa chama cha Humanist cha Nigeria mwenye umri wa miaka 37, alikiri mashtaka yote 18 na kuomba ahurumiwe.


Amekuwa kizuizini tangu 2020. Kundi lmoja la Kislamu liliwasilisha ombi kwa mamlaka likimtuhumu Bala kwa kuchapisha ujumbe wa kejeli kuhusu Uislamu kwenye mitandao ya kijamii.


Kano ina idadi kubwa ya Waislamu. Ni mojawapo ya majimbo 12 kaskazini mwa Nigeria ambapo sheria ya Kiislamu inatekelezwa pamoja na sheria za nchi.


Bala angekabiliwa na hukumu ya kifo ikiwa angeshitakiwa katika mahakama ya Kiislamu.


Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu yamelaani kuzuiliwa kwake na kutaka aachiliwe.


Bala alikana imani yake ya Kiislamu mwaka wa 2014. Kisha aliripotiwa kupelekwa katika hospitali ya magonjwa ya akili kabla ya kuruhusiwa.


Alikamatwa mwaka wa 2020 katika jimbo jirani la Kaduna, na kuhamishiwa Kano, jimbo lake la nyumbani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.