Roman Abramovich amelazimishwa kuuza klabu ya Chelsea FC na kuihahamisha mashua yake ya kifahari nje ya maji ya nchi za Muungano wa ulaya.
Mali za birionea wa Mrusi Roman Abramovich zenyethamani ya dola bilioni 7 (£5.4bn) zinazohusiana naye zimefujwa na mahakama yaJersey.
Jumanne, polisi ya Jersey ilisaka eneo linaloshukiwa kuwa na shuguli za kibiashara zenye uhusiano na Bw Abramovich katika kisiwa hicho, Maafisa wa idara ya sheria ya walisema.
Bilionea Abramovich yuko katika orodha ya vikwazo vya Uingereza vinavyohusiana na vita vya Urusi katika Ukraine.
Kisiwa cha Channel Island Jersey kinafuata sera ya Uingereza na kuwawekea vikwazo watu walioko kwenye orodha hiyo ya Uingereza.
"Mahakama hiyo pia iliweka amri rasmi tarehe 12 Aprili, inayofahamika kamasaisie judiciaire, juu ya mali zinazofahamika kuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 7 za Kimarekani ambazo zinashukiwa kuwa na uhusiano na Bw Abramovich na ambazo zinapatikana Jersey au zimeingizwa katika taasisi zaJersey," Maafisa idara ya sheria wa Jersey walisema.
Bw Abramovich alikuwa ni miongoni mwa matajiri Warusi walioongezwa mwezi uliopita kwenye orodha ya uingereza na muungano wa Ulaya ya vikwazo , ambao tayari wamekwishachukuliwa hatua ya kuchukuliwa kwa mashua zao za kifahari na mali zao nyingine za kifahari.
Bilionea huyo alijaribu kuuza klabu ya soka ya Chelsea katika mwezi March, lakini mchakato huo uliondolewa mikononi mwake na serikali baada ya kuwekewa vikwazo.
Mapema mwezi huu, taifa la Caribbean la Antigua and Barbudalilisema liko tayari kuisaidia Uingereza kushikilia mashua zinazomilikiwa na Abramovich.
Boti hizo za kifahari zilizohusishwa na mfanyabiashara Abramovich, kwa pamoja zina thamani inayokadiriwa kuwa ya dola bilioni 1.2 na kwa sasa zimetia nanga kusini mwa Uturuki, nje ya eneo la Muungano wa Ulaya na uingereza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.