Serikali imesema ipo mbioni kuvifungulia vyombo vya habari ambavyo bado vimefungiwa mara baada ya kumaliza mazungumzo yanayoendelea hivi sasa baina ya mamlaka na wahusika.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne, Desemba 7, 2021 na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju wakati akizindua kikao kazi cha Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kinachofanya marejeo na kuchambua mapendekezo 252 ya haki za binadamu.Mpanju amesema lengo la Rais Samia ni kuhakikisha anarejesha uhuru wa vyombo vya habari nchini.
“Hili ni miongoni mwa mapendekezo mliyoyatoa, itakapofika Februari 14 tutasimama na kutaja mapendekezo ambayo Serikali itakuwa imeyakubali na mpaka sasa tayari mengi yameshafanyiwa kazi likiwamo la wasichana wanaopata ujauzito wakiwa shuleni.
“Uhuru wa vyombo vya habari ni jambo ambalo Rais Samia Suluhu Hassan amelisimamia na anahitaji matokeo ya haraka. Tumeshakutana na wadau na jana tumekutana na mamlaka husika kupitia vifungu vyote kuhakikisha kwamba tunavifungulia vyombo vyote vya habari ambavyo vilifungiwa. Rais ameagiza lazima tumalize hili jambo,” amesema Mpanju.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.