Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mkazi wa mtaa wa Kanisani B uliopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe anaefahamika kwa jina la Raban Razalo (48) amefariki kwa kujinyonga na waya kwa madai ya kutoridhishwa na kitendo cha Pandree wa kanisa la Moravian kushindwa kumtaja jina wakati wa misa ya sadaka ya shukrani iliyofanywa na mkewe baada ya mtoto wao wa miaka 10 kupona majeraha ya kuvunjika mguu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema taarifa zilizobainiwa na jeshi hilo ni kwamba mtoto wa familia hiyo mwenye umri wa miaka 10 alivunjika mguu na kupelekea familia kuzunguka katika hospitali tofauti kupata matibu na kisha kupona jambo ambalo limemsukuma mama kwenda kanisani kutoa sadaka ya shukrani ambayo imekuwa chanzo cha kuondoa maisha ya baba wa familia .
“Walivyoenda kutoa sadaka ya shukrani,Pandree wa kanisa hilo amemtaja mama wa mtoto peke yake,baba imemletea sintofahamu na matokeo yak e baba ameamua kujinyonga kwa kutumia waya wa TTCL
Kamanda Issa ametoa wito kwa viongozi wa dini kuangalia umuhimu wa familia kwa kuwa inaundwa na baba na mama.
“Viongoizi wa dini angalieni umuhimu wa familia,familia ni baba na mama,ukimtaja mmoja matokeo yake ndipo unapopata sintofahamu na maamuzi yasiyo kuwa na tija”amesema kamanda Issa
Aidha ametoa rai kwa wanafamilia kuto chukua maamuzi kwa jambo amablo wamekwazika huku akisikitika kwa familia hiyo kumuuguza mtoto mpaka kupona na baadaye mzazi anafariki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.