ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 26, 2021

WAWILI WAHUKUMIWA KUNYONGWA NJOMBE.

 


Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imewahukumu washtakiwa wawili, Mwapulise Mfikwa (29) na Manase Mhada (25) kunyongwa hadi kufa baaba ya kukutwa na hatia ya mauaji ya kukusudia ya Eva Mgaya.


 Mahakama hiyo ambayo imekaa kikao chake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe imetoa hukumu hiyo leo Ijumaa Novemba 26, 2021.


Akisoma hukumu hiyo leo mbele ya Mahakama hiyo katika shauri la jinai namba 2/ 2018, Jaji Firmin Matogolo amesema washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume cha sheria kifungu cha 196 na 197 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2019.


Amesema Mei 8, 2015 washtakiwa hao walikwenda nyumbani kwa mume wa marehemu ambaye ni Wilfred Ng'olo wakiwa na bunduki aina ya shotgun iliyotengenezwa kwa kienyeji.


Amesema walifika na kuvamia, kuiba na kunyang'anya fedha nyumbani kwa marehemu huyo.


Amesema washtakiwa walichukua simu ya mume wa marehemu na kumpiga risasi Eva Mgaya kwa kutumia bunduki hiyo na kusababisha kifo chake papo hapo.


"Mshtakiwa wa kwanza alikamatwa porini akiwa na bunduki hiyo iliyotumika katika mauaji hayo" amesema Jaji Matogolo.


Mawakili wa Serikali waliokuwa upande wa Jamhuri kwenye kesi hiyo ya jinai Matiku Nyangero na Andrew Mandwa wamesema kutokana na kosa walilofanya washtakiwa hao mahakama hiyo itoe adhabu kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya makosa ya jina kifungu namba 196 na 197 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2019.


Pia waliiomba mahakama hiyo kumrejeshea mume wa marehemu simu iliyoporwa na washtakiwa hao pamoja na kurejesha silaha hiyo jeshi la polisi ili isijeleta madhara kwa wananchi.


Mawakili kwa upande wa utetezi, Octavian Mbungali na Jerome Njiwa wamesema wamekubaliana na hukumu na maamuzi ya mahakama hiyo kutokana na kosa hilo kutokuwa na adhabu mbadala zaidi ya hukumu ya kunyongwa hadi kufa.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.