ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 22, 2021

SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA HUDUMA YA MENO

 


Na WAMJW-DSM 

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima amesema serikali ya awamu ya sita  imejipanga kuboresha huduma katika sekta ya afya ikiwemo idara ya kinywa na meno ambapo hospitali 28 za Rufaa katika mikoa zimepatiwa vifaa tiba na dawa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa kwenye maeneo yao ili kupunguza gharama kwa jamii  katika kutafuta huduma. 


Amesema hayo leo 22.11.2021 jijini Dar es esalam katika kikao kazi cha Madaktari wa kinywa na meno wa mikoa na hopitali za Halmashauri kwa lengo la kujadili jinsi ya kuboresha mfumo mzima wa utoaji wa huduma za Afya, kutathimini hali ya utekelezaji wa sera, mipango na miongozo iliyopo, kuimalisha upatikanaji wa takwimu na usimamizi wa utoaji wa huduma za afya idara ya kinywa na meno hapa nchini.

Aidha, Dkt Gwajima amesema  Serikali imetoa ajira kwa watumishi 10 wa kada za Afya kinywa, wateknolojia wa maabara watano, Madaktari watano wa kinywa na meno wameajiliwa katika hosoitali za Rufaa Mikoa.

Amesisitiza kuwa, Serikali imeongeza vituo vya kutoa huduma za Afya kinywa na meno 315 kati ya 6,150 vinavyomilikiwa na Serikali ambapo vituo 22 vipya vimeanzishwa, Zahanati moja, Vituo vya Afya 12 na Hospitali 9 na vya kutolea huduma za Afya kinywa na meno kwa lengo la kusogeza huduma kwa jamii. 


Amesema, Serikali inamikakati ya kufikisha huduma za kinywa na meno kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2025 ili kuwapunguzia wananchi kutembea umbali mrefu ambapo imebainika wilaya ya chunya mkoa wa mbeya wananchi wanatembea umbali wa kilometa 200 kutoka zahanati ya Kambikatoto kwenda hospitali ya Wilaya Chunya hali ambayo inassbabisha usunbufu kubwa kwa jamii


Aidha Dkt Gwajima amewataka wananchi kubadilisha tabia ikiwemo kupiga mswaki kwa kutumia dawa yenye madini ya Floride ili kuimarisha fizi kwa lengo la kupunguza ung'oaji wa meno ambapo takwimu za kitaifa zinaonyesha mwaka 2020  kulikuwa na wagonjwa wa kinywa na meno 662,341 huku wagonjwa waliotoboka meno wakitajwa kuwa 507,508 sawa na asilimia 77 ya wagonjwa wote na wenye matatizo ya fizi wagonjwa 63,776 hali hii inaonesha taifa linakabiliwa kuwa na wagonjwa wengi wa kinywa na meno.



Kwa upande wake Mratibu wa Afya ya Kinywa ba Meno Nchini Dkt Baraka Nzobo ameionba serikali kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya kununua wa dawa na vifaa tiba kila mkoa kwa lengo la kuongeza uzalishaji mali ili kuongeza mapato ya serikali kwa kupata faida ya shilingi milioni 50,000 hali itakayosaidiakupata dawa na vifaa kwa wagonjwa wa misamaha.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.