ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 24, 2021

MAGDALENA ANDERSON NI MWANAMKE WA KWANZA KUCHAGULIWA KUWA WAZIRI MKUU SWEDEN

 

Bunge la Sweden leo limemuchaguwa kiongozi wa chama cha Social Democratic na waziri wa sasa wa fedha Magdalena Anderson kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke, baada ya Anderson kufikia makubaliano ya kuunda serikali katika dakika za mwisho.


Anderson atachukuwa nafasi ya waziri mkuu anayeacha madaraka Stefan Lofven baada ya jumla ya wabunge 117 kumchaguwa, 57 hawakupiga kura, nao 174 hawakumchaguwa.


Lofven alijiuzulu Novemba 10 baada ya kuongoza serikali kwa miaka 7 kama waziri mkuu, hatua ambayo ilitarajiwa ili kumpa mrithi wake muda wa kutosha kujianda kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao ambao utafanyika Septemba mwaka ujao wa 2022


Chini ya mfumo wa kisiasa wa Sweden, mgombea kwenye wadhifa wa waziri mkuu haitaji kuungwa mkono na wabunge wengi, anahitaji tu kutokuwa na wingi wa kura au kura 175 dhidi yake.



Anderson mwenye umri wa miaka 54, ambaye alichukuwa wadhifa wa kiongozi wa chama cha Social Democrats mapema mwezi huu alifikia makubaliano ya kuunda serikali na chama cha mrengo wa kushoto Jumanne, juu ya kuongeza pensheni ili aungwe mkono katika kura ya Jumatano bungeni.


Awali, alipata uungwaji mkono wa vyama shirika vya Social Democrats, kile cha kutetea mazingira, the Greens na chama cha mrengo wa katikati.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.