Gari lilobeba mwili wa aliyekuwa mpigapicha wa Ayo Tv Mwanza, marehemu Nelson Brigeri ‘Nelly TZA likiwa kwenye msafara kutoka nyumbani kwao Kanyerere wilayani Nyamagana mkoani Mwanza kuelekea makaburi ya Kanyerere.
Sehemu ya umati uliojitokeza makaburi ya Kanyerere.
Jeneza lililoubeba mwili wa aliyekuwa mpigapicha wa Ayo Tv Mwanza, marehemu Nelson Brigeri ‘Nelly TZA likiwasili katika makaburi ya Kanyerere.
Mkurugenzi wa Ayo Tv, Bwana Millard Ayo (aliyeshika picha) alikuwa mmoja wa washiriki kwenye mazishi hayo ya aliyekuwa mpigapicha wa Ayo Tv Mwanza, marehemu Nelson Brigeri ‘Nelly TZA.
Kwaheri Nelson Brigeri ‘Nelly TZA
Marafiki mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kuuaga na kukamilisha safari ya mwisho ya pumziko la milele yake marehemu Nelson Brigeri ‘Nelly TZA aliyefariki kupitia ajali mbaya ya gari iliyotokea eneo la Kibaha usiku wa kuamkia tarehe 18 Agasti 2021 baada ya kugongana uso kwa uso na gari la mizigo.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Nelson Brigeri ‘Nelly TZA likishushwa kaburini.
Safiri salama Nelson Brigeri ‘Nelly TZA
"Binadamu ni mavumbi na mavumbini tutarejea, safiri salama Nelson Brigeri ‘Nelly TZA"
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe Sima Costantine alikuwa ni miongoni mwa walioshiriki mazishi ya mwanahabari wa Ayo Tv Mwanza, Nelson Brigeri ‘Nelly TZA
Wanafunzi toka shule mbalimbali za jijini Mwanza nao walioshiriki mazishi ya mwanahabari wa Ayo Tv Mwanza, Nelson Brigeri ‘Nelly TZA
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.