Na Maridhia Ngemela
Mganga mfawizi wa hospitali ya rufaa Mkoa sekou toure Bahati Peter Msaki amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata chanjo na kuachana na maneno ambayo yanasemwa kwenye mtandao ya kijamii
Msaki ameeleza hayo wakati wa zoezi la uzinduzi wa chanjo ya kinga ya ugonjwa wa uviko 19 iliyozinduliwa leo mkoani hapa amesema zaidi ya watoa huduma 200wamejiandikisha kw lengo la kupata kinga huyo kwani ni kundi moja wapi ambalo limepewa kipaumbele kutokana na kazii inayowakutanisha na watu mbalimbali.
Bahati ameeleza kuwa kinga ni bora kuliko kusubiri kuungua ndio ukapate matibabu hivyo hakuna sababu ya kuendelea kudanganyana juu ya chanjo kuwa ina madhara mwilini.
Aidha amewataka wananchi kuendelea kujikinga kwa kuchukua hatadhali kwa kivaa barakoa, kunawa mikono na kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima.
Kisali Simba ni mmoja kati ya waandishi wa habari aliyejitokeza kupata chanjo ameeleza kuwa hakuna changamoto yeyote ambayo ameipata baada ya kupata kuchanjo hiyo ya Uviko 19 .
"Nimefurahi kupata chanjo hii kwani kuanzia sasa niko imara kabsa sina hofu juu ya maambukizi ya ugonjwa huu" alisema kisali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.