Jukwaa la walimu Wazalendo Halmashauri ya jiji la Mwanza nchini Tanzania limetoa mifuko 240 ya saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Bulale.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk Philisi Nyimbi, katibu wa jukwaa hilo, Lucas Kondoko amesema wameguswa na adha wanayoipata wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu.
Amesema saruji hiyo yenye ya Sh4.2 milioni imepatikana baada ya kuchangishana ili kuwanusuru wanafunzi hao.
Dk Nyimbi amewapongeza walimu hao kwa hatua waliyoichukua na kuwataka watumishi wengine kuiga mfano huo,
Nae Kaimu mkurugenzi wa Jiji hilo, Dandford Kamenya amesema watahakikisha saruji hiyo inafanya kazi iliyokusudiwa ili kupunguza tatizo la ukosefu wa sehemu za kusomea.
Kata ya Buhongwa yenye mitaa 18 ina wakazi 32, 000 ikiwa na shule za msingi tatu na sekondari moja ambayo licha ya kudaiwa kuzidiwa wingi wa wanafunzi lakini ipo mbali na wanafunzi hulazimika kutembea zaidi ya kilometa 10 kufuata.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.