ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 13, 2020

NI HUZUNI KUU NA VILIO MOTO WATEKETEZA MITAJI YA MACHINGA MAKOROBOI


Moto uliozuka saa 9 alfajiri ya Jumatano Februari 12, 2020 katika soko la Makoroboi mkoani Mwanza umeacha simanzi kwa wafanyabiashara kutokana na bidhaa zao kuteketea. Moto huo uliowaka kwa dakika takribani 45  ulizimwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi, hakuna bidhaa zilizookolewa. Baadhi ya wafanyabiashara wamekiri kuwa biashara walizokuwa wakifanya katika eneo hilo zilikuwa msingi wa kuendesha maisha yao, huku Timoth Clemence akisema kuwa taarifa za kuzuka kwa moto huo alizipata baada ya kupigiwa simu na kusababisha apate mshtuko bila kujua la kufanya. Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,  Dk Philis Nyimbi amethibitisha amewataka wafanyabiashara kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vinaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo. Naye Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro amezungumza. Bidhaa za wafanyabiashara wadogo 159 zimeteketea huku mabanda 65 nayo yakiteketea. #JembeFm #JembeHabari #KAZINANGOMA #DriveMix @jembefm

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.