ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 4, 2019

KIKONGWE ASHAMBULIWA KWA FIMBO HADI KUFA.



Na Amiri kilagalila-Njombe

Jeshi la polisi mkoani Njombe limethibitisha kuuwawa kwa mzee Issa Pila(80) ambaye alishambuliwa kwa fimbo na wanafunzi wa shule ya msingi Uganga iliyopo tarafa ya Bulongwa wilayani Makete mkoani Njombe kwa tuhuma za ushirikina.

Akizungumzia  tukio hilo lililotokea octoba 28 kamishna msaidizi wa polisi ACP Hamisi Issa amesema taarifa zilizopatikana mara baada ya kufanya mahojiano na wanafunzi wa shule hiyo pamoja na wanakijiji zinasema wanafunzi walichukua uamizi wa kumshambulia mzee huyo baada ya kuona akichuma majani katika eneo la shule na kuwanyoshea vidole jambo ambalo liliibua hasira na kuamua kumkimbiza na kisha kumkamata na kuanza kumuadhibu.

Kamanda huyo pia amesema katika uchunguzi wa awali wamebaini kijiji hicho kimetawaliwa na imani kubwa za kishirikiana ambao umekuwa ukifanyika katika mazingira ya waziwazi kwakuwa hata wakati timu ya upelelezi ilipotumwa kufanya uchunguzi wanafunzi waliokuwa wakihojiwa wanapofikia hatua ya kutoa taarifa sahihi walikuwa wakizimia .

Katika taarifa nyingine ambazo zimepatikana kutoka kwa walimu na wanafunzi ni kwamba kumekuwa na viashiria vingi vya vitendo vya kishirikina hata kabla ya kutokea kwa mauaji ya kifo hicho  ambapo inaelezwa kumekuwa na matukio ya nusu ya wanafunzi kuzimia wakati wa kipindi bila ya sababu inayoeleweka shuleni hapo hatua ambayo imekuwa ikileta hofu kwa walimu.

Kuhusu hatua zilizochukuliwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa anasema jeshi la polisi linamshikilia mtu mmoja ambaye anatupiwa lawama na watu wengi kuwa miongoni mwa washirikina wanaotekeleza vitenzo hivyo vya kichawi huku wwengine wakidaiwa kukimbia wakihofia kutiwa nguvuni kwa mahojiano huku pia akidai hata madai ya wanafunzi kujieleza wazi kwamba wamefanya mauaji hayo wanayatilia shaka kwa kuwa wamekuwa wakipigwa mapepo na kuongea mambo yatofauti pindi wanapo hojiwa kuhusu kufanya kitendo hicho.

Aidha kamanda amesema Timu ya uchunguzi bado inaendelea na kazi ya kubaini wahusika halisi wa tukio la mauaji ya kikongwe huyo baada ya kupata shaka kuhusu uhusika wa wanafunzi hao kwa kuwa kila wanapofanya mahojiano na wanafunzi wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji wanapokaribia kusema ukweli wamekuwa wakipandisha mashetani na kuanza kutoa taarifa zisizo eleweka na kuonyesha ishara mbalimbali zinazodaiwa kuhusiana na ushirikina.

Mganga mfawidhi wa zahanati ya Uganga Frank Gavana alithibitisha pia kutokea kwa kifo ambapo alidai kuwa uchunguzi wa mwili ulibaini marehemu alikuwa na majeraha sehemu za kichwa 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.