ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 14, 2019

MBUNGE MTATURU AWAPA NENO VIJANA 500 WANAOTEMBEA KUMUENZI NYERERE NA KUMUUNGA MKONO RAIS DK MAGUFULI KWA UCHAPAKAZI WAKE AKITEKELEZA NDOTO YA HAYATI BABA WA TAIFA
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (CCM) akizungumza na vijana wa CCM kutoka Wilaya ya Chato waliotembea km 115 kutoka Wilaya ya Geita Mjini hadi Wilaya ya Chato kumbukizi ya miaka 20 ya logo cha Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere na kuunga mkono uthubutu wa Rais Dk John Magufuli, Rais wa serikali  ya awamu ya tano ya kutekeleza miradi mikubwa iliyoachwa na Mwl kwa vitendo ikiwemo mapambano ya rushwa, uhujumu uchumi na maendeleo na upatikanaji huduma bora. PICHA NA PETER FABIAN.

NA MWANDISHI WETU, CHATO.

VIJANA 500 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotembea kilomita 115 kutoka Wilaya ya Geita Mjini hadi Wilayani Chato kumuenzi na kumkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere pamoja na kumuunga mkono Rais Dk John Pombe Magufuli kwa kuthubutu kutekeleza miradi mikubwa ikiwa ni kutekeleza ndoto za mwalimu Nyarere.

Matembezi hayo yaliyoanza  Oktoba 9 na kuhitimishwa leo Oktoba 14 siku ya kumbukumbu ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwl Nyerere ambaye anatimiza miaka 20 tangu alipofariki kwenye Hospitali ya kimataifa ya Mtakatifu Thomas Nchini Uingereza.

Akitoa hamasa kwa vijana 500 waliokuwa wamefika eneo la kituo cha Shule ya Msingi Bwanga Wilayani Chato, Mgeni rasmi aliyealikwa na kupata fursa ya kuongea na vijana hao jana Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (CCM) alipongeza vijana hao na kuwataka kuendelea kumuenzi Mwl Nyerere kwa vitendo ambavyo alivipiga vita kwenye utawala wake.

"Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere alipinga na kukataa rushwa, wezi wa rasilimali za Taifa (wahujumu uchumi), watu waliotafuta uongozi kwa lengo la kutugawa kwa ukabila, dini na mahali tunapotoka, waliojilimbikizia mali na waliotumia madaraka kwa masilahi yao binafsi huku rasilimali za madini, ardhi maliasili za hifadhi za Taifa,  maziwa na mito itumike kuwanufaisha watanzania wote bila kuwabagua," alisema.

Mtaturu alisema Rais Dk John Magufuli amethubutu kumuenzi Hayati Baba wa Taifa katika uongozi wake kwa kutekeleza mradi mkubwa wa umeme mto Rufiji, kuboresha ujenzi wa Reli ya kisasa ya Kati na kufufua , usafiri wa anga (ununuzi wa ndege), ujenzi wa Meli mpya Ziwa Victori, Nyansa, Tanganyika, utolewaji Elimu bure, ujenzi wa Hospitali mpya za Wilaya 67 na Vituo vingi vya Afya, barabara za lami na madaraja likiwemo la Kigongo-Busisi bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Nchi ya Uganda na Rais Dk Magufuli ameonyesha kupiga vita rushwa, kuchukua hata kali kwa wahujumu uchumi na wanaotaka kuwagawa watanzania kwa siasa za ukabila, dini na maeneo tunayotoka," alisema.

Mbunge huyo Rais Dk Magufuli anatembea na kufuata misingi ya Hayati Mwl Nyerere kwa vitendo, amethubutu kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa ndoto ya Mwl Nyerere lakini upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu, majisafi, umeme na miundombinu ya barabara za lami, changalawe na usafiri wa anga (ndege), reli kukuza kilimo, ufugaji bora na kuimalisha sekta ya viwanda na mawasiliano haya yametekelezwa kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

"Tangu uongozi wa serikali ya awamu ya tano wa chini ya Rais Dk Magufuli Mzalendo ambaye amewagusa watanzania kwa uchapakazi wake na kuthubutu kusimamia bila woga rasilimali za Taifa ikiwemo madini na kuchukua hata kali kwa wahuhumu uchumi na sasa amerejesha nidhamu kwa watumishi serikalini iliyokuwa imeteteleka na hata kudhibiti wanasiasa waliolenga kulivuruga Taifa kwa masilahi yao binafisi na vibaraka wa mataifa ya Nje lakini kuendelea kusimamia misingi ya Amani na Umoja wa kitaifa uliowekwa na waasisi wa Taifa hili Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abed Aman Karume tangu walipotuunganisha," alisema

Katibu wa CCM Wilaya ya Chato, Acheni Maulidi alisema kwamba katika kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwl Nyerere kwa vitendo wameanda matembezi hayo pia kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC, kutekeleza miradi mikubwa ambayo Hayati Baba wa Taifa alikusudia kuitekeleza au kuona inatekelezwa lakini pia kuhamasisha wananchi kumuunga mkono Rais ikiwemo kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuchagua viongozi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji katika maeneo ya.

" Pamoja na Rais kuthubutu kutekeleza ndoto za Hayati Baba wa Taifa Mwl Nyerere lakini ametuonyesha watanzania kuwa Mzalendo aliyeamua kulitumikia taifa kwa uadilifu na kurejesha misingi ambayo ilianza kuwekwa kando na viongozi na watumishi wa umma hali iliyopelekea kuanza kumomonyoka kwa maadili ya watumishi wa umma serikalini na wanasiasa kuanza kulivuruga taifa kwa masilahi yao bila kutambua kuwa Amani na Umoja ndiyo nguzo ya misingi ya taifa letu," alisema.

Katibu Maulidi alishukuru watu na wadau waliounga mkono na waliochangia vitu mbalimbali kufanikisha matebezi hayo ya km 115 ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwl Nyerere pia kuwataka watanzania wote bila kujali Itikadi zao za kisiasa, dini, makabila na maeneo watokayo kuendelea kumuombea Rais Dk John Magufuli aendelee kuliongoza Taifa kwa uzalendo, busara na hekima ili watanzania wote tupate huduma bora na maendeleo kama ilivyokuwa ndoto ya Muasisi na Baba wa Taifa.

Maulidi alisema kwamba kupitia matembezi ya vijana hao kumelenga pia wananchi wa maeneo mbalimbali ya vijiji na vitongiji kujitokeza kujiandikisha na kuwapa fursa wananchi kuchaguza viongozi wa serikali za Vijiji 115 na Vitongoji 599 ambapo anamatumaini makubwa kwa CCM kuibuka na ushindi wa kishindo ili kumpatia zawadi ya pekee Rais Dk John Magufuli kuthubutu kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ambayo Baba wa Taifa Hayati Mwl aliomba itekelezwe licha ya kung'atuka madarakani mwaka 1985 ambapo awamu ya tano ya uongozi wa Dk Magufuli umeanza kutekeleza kwa vitendo. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.