Watu wanne wamepoteza maisha katika Kisiwa cha Siza kilichopo Wilaya Ukerewe mkoani Mwanza, kufuatia mzozo baina ya wananchi na maafisa wa kikosi cha ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria.
Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama Mkoa ambaye ndiye Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amesema tukio hilo limetokea leo Julai 22, 2019 ambapo wananchi wanne wamepigwa risasi na kusababisha watatu miongoni mwao kufariki dunia papo hapo huku mmoja akikimbizwa katika Hospitali ya Nansio kwa matibabu.
Mongella amebainisha kuwa mtu wa nne aliyefariki ni Afisa mfawidhi wa rasilimali za uvuvi Kanda ya ukerewe aliyekuwa kiongozi wa kikosi hicho chenye jukumu la kudhibiti na kutokomeza biashara haramu ya mazao ya uvuvi katika Ziwa Victoria ambaye alishambuliwa na wananchi ambapo pia askari mmoja amejeruhiwa vibaya hata kukimbizwa katika Hospitali ya Nansio kwaajili ya huduma zaidi.
Taarifa zaidi tutaendelea kuwajuza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.