Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella mwishoni mwa wiki (Ijumaa ya tarehe 22 Machi 2019) ameongoza kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa (RCC) ambacho kimepitia na kushauri mpango wa rasmi ya bajeti ya halmashauri na manispaa za wilaya mbalimbali mkoani hapa kwa mwaka 2019/2020.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Makatibu Tawala, Wakuu wa wilaya, Wenyeviti, Wakurugenzi pamoja na Wataalamu wa Sekretarieti ya mkoa, Viongozi wa vyama vya siasa, Wakuu wa idara, Maofisa tarafa, Watendaji wa Kata na Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Aidha Wajumbe wakikao hicho wamepata nafasi ya kujadili kwa uwazi rasimu ya bajeti, wameshauri miradi viporo ya muda mrefu ipewe kipaumbele katika mwaka huu na ikamilike kwa wakati.
GsengoTv inakuletea sehemu ya majumuisho upande wa hitimisho ambapo msemaji wa kwanza anayeonekana katika video ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kali na msemaji wa pili ni Mwenyekiti wa kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.
Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Mamlaka za Serikali za mitaa kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 halmashauri za Mkoa wa Mwanza zilijiwekea malengo ya kukusanya jumla ya Ts. 35,086,833,000/= Hadi kufikia mwezi Februari, 2019 Jumla ya Tsh. 21,173,018,080/15 sawa na 60.34% ya lengo.
Makusanyo hayo yameongezeka kwa Tsh. 6,340,121,731/30 sawa na asiliamia 42.74 ukilinganisha na kipindi kama hiki kwa Mwaka 2017/18.
Moja ya Changamoto katika ukusanyaji wa mapato ni pamoja na Baadhi ya wakusanyaji kutumia fedha hizo kabla ya kuingia benki na kusababisha Halmashauri kushindwa kutambua mapato hayo.
Sababu nyingine inayotajwa ni baadhi ya mashine za kielektoniki (POS) zinazotumika kukusanya mapato kuzimwa (Off-line) kwa kisingizio cha kukosa 'bundle'.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.