Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Prof. Joseph Buchwaishaija (mwenye Kaunda suti), akisisitiza jambo kwa mwakilishi wa ghala la kuhifadhi korosho la OLAM Theophil Nandonde wakati alipofanya ziara ya kukagua maghala ya kuhifadhi korosho mikoa ya Mtwara na Lindi.
Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchwaishaija, akipokea maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya OLAM inayo miliki maghala ya kuhifadhi korosho eneo la bandari ya Mtwara. Pembeni ni Naibu Katibu Makuu wa Wizara hiyo sekta ya viwanda Bw. Ludovick Nduhiye.
Meneja wa Bandari Mkoa wa Mtwara, Bw. Abdulkarim Salim akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Joseph Buchwaishaija wakati wa ziara yake ya kukagua maghala ya kuhifadhi korosho kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi. Kwenye ziara hiyo Serikali imefanikiwa kupata nafasi ya ziada ya kuhifadhi korosho zaidi ya tani elfu arobaini na nane.
Mwakilishi wa kiwanda
cha kubangua korosho cha Sunshine kilichopo Mtama, Lindi akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu,
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Pof. Joseph Buchwaishaija alipotembelea kiwanda hicho ili kubaini uwezo
wake wa kubangua korosho. (Picha na Idara ya Habari)
Kuhakikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano
inanunua korosho yote ya wakulima inatimia kabla ya kipindi cha masika
hakijashika kasi, uongozi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji umewatoa
hofu wakulima wote wa mikoa ya kusini kuwa serikali inao uwezo wa kununua na
kihifadhi korosho yote itakayonunuliwa.
Hakikisho hilo limetolewa na Katibu Mkuu, Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchwaishaija wakati
anahitimisha siku ya kwanza ya oparehseni ya ukaguzi wa maghala kwenye mikoa ya
Lindi na Mtwara.
“Ziara ya ukaguzi wa maghala inatokana maagizo ya
kikao cha tathmini ya Operesheni Korosho kilichoitishwa na Mwenyekiti wake
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga, ambapo pamoja na mambo mengine kilibaini
ufinyu wa maeneo ya kuhifadhia korosho kutoka kwa wakulima” anasema Prof.
Buchweishaija.
Kwenye ziara hiyo Prof. Buchwaishaija pamoja na
Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) Ludovick Nduhiye na maafisa wengine waandamizi wa
wizara hiyo walifanikiwa kukagua maghala ya korosho kwenye wilaya za Mtwara,
Mtama, Masasi na Nachingwea na kubaini kuwa maghala makuu na yale ya uhifadhi
yana nafasi ya ziada kuhifadhi korosho zaidi ya tani elfu arobaini na nane.
“Nachukua nafasi hii kuwatoa wasiwasi wakulima
wote kwamba, maghala na sehemu za kuhifadhi korosho zetu sio tatizo tena, na
tutahakikisha korosho zote ziliyopo kwenye AMCOS (vyama vya msingi)
tunazisafirisha haraka iwezekanavyo kabla ya msimu wa mvua kuanza.” Anasisitiza
Prof. Buchwaishaija.
Mbali na kukagua maghala ya kuhifadhi korosho,
ziara hiyo pia ilikuwa na lengo la kukutana na makumpuni ya kubangua korosho
ambayo yameonyesha nia na utayari wakati serikali itakapoanza kubangua korosho
ilizozinunua moja kwa moja kutoka kwa wakulima.
Operesheni ya ukaguzi wa maghala mikoa ya kusni inatarajiwa kuendelea kwenye
wilaya za mkoa wa Ruvuma kesho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.