NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Zaidi ya wakazi laki nne wilayani Kwimba
mkoani Mwanza, wameondokana na tatizo la ubovu wa miundombinu ya barabara,
baada ya Mbunge wa jimbo hilo Shanif Mansoor kukamilisha ujenzi wa barabara
kumi na tisa, zenye urefu wa kilometa 98.2.
Akikabidhi moja kati ya barabara hizo
katika kijiji cha Mwang’ombe, Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor, amesema
ameamua kuzijenga barabara hizo kwa gharama zake binafsi bila kugusa fedha za
mfuko wa Jimbo, ili kufungua milango ya fursa za kiuchumi kwa wananchi.
Kabla ya ujenzi barabara hizo
kukamilika, fursa za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo zilikuwa zikisuasua,
hasa kwa kuwakwamisha wakulima kushindwa kusafirisha mazao yao ya biashara
kwenda katika masoko.
Katika makabidhiano hayo mkuu wa wilaya
ya Kwimba Senyi Ngaga, amemshukuru Mbunge huyo kwa jitihada zake, huku
akiwahimiza wananchi kuchangamkia fursa za kibiashara, kwa kuwa vikwazo
vilivyokuwa vikiwakabili kiuchumi vimetoweka.
Akipokea barabara hizo kwa niaba ya
serikali.mkuu wa wilaya kwimba mkoani Mwanza mhe.SENYI NGAGA,pamoja na meneja
wa wakala wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Edwin Madoshi, amemshukuru
Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor, ni mfano wa kuigwa kwa juhudizake za
kuchochea maendeleo katika jimbo la kwimba.huku akiwataka wadau wengine kuunga
mkono jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.
Wakati ujenzi wa barabara hizo ukiwa
unalenga kutekeleza ilani ya Chama cha mapinduzi (CCM) kwa wananchi, miradi
mingine ya kijamii ambayo tayari imeshakamilishwa na mbunge wa Jimbo hilo, ni
ujenzi wa vituo vya afya, uboreshaji wa miundombinu ya sekta ya elimu, Maji na
umeme.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.