GSENGOtV
Katika siku ya pili mara baada ya mafunzo kwa vitendo ya jinsi ya kumkwamua mtoto wa kike toka kwenye wingu la ukatili na mbinu ya jinsi ya kuvidhibiti, viongozi wa kada mbalimbali washiriki wanatinga katikati ya Soko kuu wilayani Sengerema, na kulianzisha.
'Vigogo' hao waliitoa akili na kuanza kuyarudi magoma hadharani kiasi cha kuwafanya watu sokoni hapo kukusanyika eneo la tukio wasijue kimewasibu nini, nao walipoona umati umekaa sawa sawia na matamanio yao, wakaliamsha igizo moja matata lenye funzo ndani yake na mwishowe ikawa ni zamu sasa kwa wao 'kuchonga' na raia walizuka sokoni hapo.
Mpango wa kuielimisha jamii kwa kutumia maigizo kupitia watu maarufu na wanaotambulika katika nyadhifa mbalimbali kwenye jamii na ngazi mbalimbali serikalini, umekuja kama mbinu mpya kukabiliana na yale yanayochangia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hususani mtoto wa kike.
Badala ya kutumia vikundi vya sanaa, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Mabwana na Mabibi afya, Wachungaji, Mashekhe, Viongozi jumuiya ya wazazi, Makatibu Tawala, Wenyeviti na Makatibu Watendaji wa vijiji na vitongoji ndiyo wamekuwa wasanii.
Ni katika mradi wa mwaka mzima uliochini ya FAWE Tanzania, ukiratibiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.