Picha kwa hisani ya mtandao. |
Mahakama Kuu imetupilia mbali mapingamizi ya upande wa mashtaka dhidi ya rufaa ya dhamana ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Sam Rumanyika ambaye amesema hana uhakika iwapo mapingamizi ya serikali yalikuwa na nia ya kuchelewesha usikilizwaji wa rufaa ambayo itaanza kusikilizwa leo saa 8 mchana.
Mbowe na Matiko waliwasilisha rufaa mahakama kuu kupinga Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana wiki iliyopita kwa tuhuma kuwa walisafiri nje ya nchi bila idhini ya mahakama hiyo na hivyo kukiuka masharti ya dhamana.
Mbowe, Matiko na viongozi wengine saba waandamizi wa CHADEMA wanakabiliwa na kesi ya jinai katika Mahakama ya Kisutu wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukusanyika kinyume cha sheria mwezi Novemba mwaka jana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.