Kampuni ya Coca-Cola, kupitia show yake ya muziki, Coke Studio Africa, inatangaza kurejea kwa msimu mpya ambao umepangwa kurushwa hewani Februari 2019. Utayarishajiwa Coke Studio Africa 2019 ushaanza kufanyika katika studio za Super Sport kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi wa Novemba 2018.
Meneja wa Mradi wa Coke Studio Africa: Andrew Endovo Alovi amesema, “Tunafuraha punde tutaanza utayarishajiwa Coke Studio Africa 2019 ---tutegemee mabadiliko ya kuvutia ya mandhari na muingiliano wamuziki. Shoo hii imekuwa mstari wa mbele kutengeneza muziki wenye ubora na wakati huo huo kuwapatia wasanii mbali mbali katika bara letu uzoefu mkubwa, na kutengeneza nafasi za kushirikiana miongoni mwao. Pia kuweza kufanya kazi na baadhi ya wasanii wa ndani na wa kimataifa wenye uweledi katika dunia ya muziki.”
Mengi kama orodha ya mwisho ya wasanii watakao shiriki itatolewa ndani ya siku chache, tunafuraha kwamba shimo la wasanii vijana mahiri katika bara letu kwa kiasi kikubwa limekuwa na sasa tunao nyota wengi wa kuwaleta pamoja na kutengeneza ushirikiano wa kushangaza na dunia kuona na kusikia. Wasanii wata oanishwa pamoja na watayarishaji wakubwa wa Coke Studio Africa, ambao wataenda kupewa jukumu la kutengeza shoo yenye mchanganyiko mzuri wa muziki na ushirikiano.
Monali Shah, Mkuu wa Maudhui na Ubora wa kampuni ya Coca-Cola upande wa Kusini na Mashariki mwa Afrika kibiashara amesema, “Tumefurahi sana kupata washirika wapya ambao wameungana nasi tunapo tengeneza muziki mkubwa kutoka Afrika kufika duniani. Sankara Hotel watakuwa washirika rasmi wa Ukarimu kwa msimu huu mpya. Ikiwa kama hoteli iliyopiga hatua na kukumbatia sanaa, tumefurahi kwamba wamekuja mezani na kuungana nasi kwenye hii safari.”Aliongeza kuwa “Pace Africa, ambao walibuni nakutengeneza safu ya vifaa vya sauti kama PACE FOCUS na PACE MATE wataipa nguvu sauti kwa msimu huu wakitupatia ‘headphones na earphones” vyote kwa ajili ya uzalishaji na baadhi ya kwaajili wateja wetu watakao bahatika.” Washirika wengine ni Yallo Leather and Home 254.
Sehemu ya kwanza ya Coke Studio Africa 2019 inatarajiwa kurushwa Februari 2019 lakini kabla ya hapo, kipindi kitaachia Kiupekee na maudhui ya awali mtandaoni na kwenye Televisheni ikiwa na mandhari ya msimu wa Christmas.
MAONI YA MHARIRI
Coke Studio Africa ni shoo isiyo ya mashindano yamuziki, ambayo inataka kuleta pamoja, nakusheherekea utofauti wa muziki wa Afrikana na vipaji. Pia ina wapa nafasi wasanii wanao chipukia kufanya kazi na baadhi ya wakali wenye vipaji toka ndani na kimataifa. Wasanii wanatolewa toka kwenye aina mbali mbali za muziki, muda na maeneo tofauti na kuwekwa kwenye jozi (kuoanishwa) ili kutengeneza muziki wa kisasa na halisi wenye sauti nzuri za Kiafrika kupitia mchanganyiko wa muziki. Jinsi wasanii watakavyo husiana na kutengeneza muziki utakao wekwa kwenye kumbukumbu na watayarishaji. Pia watapata nafasi ya kujifunza kuhusu muziki wa kila mmoja na mitindo wakati wakibadilishana tamaduni. Shoo inampeleka mtazamaji ndani ya studio ya kurekodi na kutazama mchanganyiko wa wasanii mbalimbali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.