ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 29, 2018

RAIS MAGUFULI AMJIBU ZITTO NA WAFANYABIASHARA.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametolea maelezo sakata la zao la korosho ambapo amesema kuwa endapo wafanyabiashara watakataa kununua kwa bei elekezi ya Tsh 3000 kwa kilo.

Akizungumza na wafanyabiashara wa korosho Ikulu jana Oktoba 28, 2018  Rais Magufuli amewataka wafanyabiashara kununua korosho kwa bei isiyopungua elfu 3000 na kama watakataa basi serikali ipo tayari kununua.

“Kama hamtaki kununua Korosho kwa bei ya maslahi kwa wakulima, Serikali itazinunua kwa bei nzuri na tutazihifadhi, nipo tayari hata kutumia majeshi yetu kununua Korosho na tutatafuta masoko ya uhakika ili tuuze kwa bei nzuri.“amesema Rais Magufuli.

“Serikali ina hela, inaweza kununua Korosho za wakulima wa Lindi na Mtwara kwa siku mbili. Tumenunua ndege, tumejenga reli, hatuwezi kushindwa kununua Korosho,“ameeleza Magufuli.

Wakati tamko hilo likijiri hapo jana, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliongelea sakata hilo akitaka serikali itoke hadharani kueleza sakata hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.