ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 23, 2018

KIKWETE ATUA IKULU, AMTAKA RAIS MAGUFULI AZIDI KUKANDAMIZA.




Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete leo Oktoba 23, amemtembelea Rais Dk John Magufuli Ikulu na kufanya nae mazungumzo .

Baada ya mazungumzo yao Mstaafu Kikwete amesema wamekutana kwa utaratibu wa kawaida wa kusalimiana na kutakiana heri katika majukumu.

" Nimekuja tu kumsalimia siku nyingi hatujaonana, kumtakia kila la heri, anafanya kazi nzuri, aendelee tu kukandamiza, aendelee tu kuchapa kazi na sisi tupo kwa namna yoyote tu akihitaji msaada sisi tupo tayari," amesema Rais Mstaafu Kikwete.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.