ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 11, 2018

KAZI DARASA - TUNAIANGAZIA SIKU YA UGONJWA WA AFYA YA AKILI DUNIANI - VIJANA WAKO PABAYA ZAIDI.

Matarajio Makubwa Kuliko Uwezo Walionao Hasa Vijana,Ndio Sababu Kubwa Inayotajwa Kuchangia Kuwapo Kwa Ugonjwa wa Afya ya Akili Katika Maeneo Mbalimbali Hapa Nchini.

Wataalamu wa Afya na Wanasaikolojia Wanasema Kuwa Ugonjwa Huo Mara Nyingi Huwakumba Vijana Ambao Wamekuwa na Majukumu Mengi na Wengine Kutaka Mteremko wa Maisha na Kuwa Tegemezi Hatimaye Wanapokwama Wanajikuta Wanaugua Ugonjwa wa Afya ya Akili.

Takwimu za Wizara ya Afya 2018 Zilizotolewa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dokta Faustine Ndugulile Zinasema Kuwa Kati ya Kadirio la Wagonjwa Laki Tano wa Akili Nchini ni Asilimia 48 Tu Ndio Wanafika Katika Vituo Vya Afya Huku Asilimia 24 Wakipelekwa Kwa Waganga wa Kienyeji na Asilimia Zinazosalia Wanapatiwa Msaada wa Kiroho na Wengine Wanabaki Wakirandaranda Mitaani.  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.