Bilionea mmiliki wa Klabu ya Soka ya Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha (61), raia wa Thailand amethibitishwa kuwa miongoni mwa watu waliofariki katika ajali ya helikopta karibu na Uwanja wa Klabu hiyo King Power juzi Jumamosi baada ya mechi ya timu yake na West Ham.
Leicester City imethibitisha kuwa, wafanyakazi wake wawili, rubani na abiria mmoja walifariki baada ya ndege hiyo kuanguka na kuteketea kwa moto majira ya saa 2:30 usiku huku mashuhuda wa tukio hilo wakisema ndege hiyo ilikuwa inamaliza kuondoka uwanjani hapo, ilianza kuyumba na kuanguka na kuwaka moto.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.