MAKETE
Mahakama ya Wilaya ya Makete Mkoani Njombe imewahukumu kifungo cha maisha gerezani Furaha Elenesti Sanga, Yusufu Sanga pamoja na Meneliki Sanga vijana wakazi wa kijiji cha Ihanga Kata ya Ukwama kwa kosa la kubaka kwa kuchangia mama mwenye umri wa miaka 38
Mwendesha mashitaka wa mahakama ya wilaya ya makete mkaguzi msaidizi wa polisi Ndg.Omary Kihenya ameiambia Mahakama kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo mnamo Tarehe 1.5.2018 huko katika kijiji cha Ihanga Kata ya Ukwama na kuiomba mahakama itoe adhabu kali kwani kosa walilo lifanya watuhumiwa linaweza sababisha kifo na ili iwe fundisho kwa wengine
Akisoma hukumu Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Makete Mh.John Mpitanjia amesema washitakiwa walitenda kosa hilo kinyume na kifungu 131 (1) (2) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2002 na kua mahakama imepitia ushahidi ulio tolewa na upande wa mashitaka na kujiridhisha pasina kuacha shaka kua washitakiwa walitenda kosa hilo na hivyo mahakama imewahukum washtakiwa kwenda jela kifungo cha maisha
Katika hatua nyingine Mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani Ajuaye Chaula mkinga mkazi wa Lupalilo kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 16 anae soma kidato cha pili shule ya Sekondari usililo
Imedaiwa Mahakamani hapo hii leo na mwendesha mashtaka wa mahakama ya Wilaya ya Makete mkaguzi msaidizi wa polisi Ndg Omary Kihenya kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo mnamo Tarehe 2.6.2018 majira ya saa 12 jioni huko katika kijiji cha Lupalilo Tarafa ya Lupalilo
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Makete Mh.John Mpitanjia amesema Mahakama imejiridhisha pasipo kuacha shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitka na kua mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130 (1) (2) (e) na kifungu cha 131 (1) cha kanuni ya adhabu kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002
Ndipo mahakama ikamtia hatiani Ajuaye Chaula kutumikia kifungo cha miaka 30 jela pamoja na viboko 12 na kumlipa fidia shilingi lakitano mhanga huku rufaa ikiwa wazi kwa mtuhumiwa.
Mahakama hiyo pia imemhukumu Victory Mgenzi Mlowe mwenye umri wa miaka 23 kwa kosa la kumbaka binti mwenye umri wa miaka 16 anae soma shule ya Sekondari Lupalilo kidato cha kwanza.
Imedaiwa pia na mwendesha mashtaka wa mahakama ya wilaya ya makete mkaguzi msaidizi wa polisi Ndg Omary Kihenya Mahakamani hapo hii leo kua mshitakiwa alitenda kosa hilo mnamo Tarehe 29 .5.2018 Saa 6 mchana huko katika kijiji cha Tandala kata ya Tandala.
Hakimu mkazi mfawidi wa mahakama ya wilaya ya makete Mh John Mpitanjia amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na akifungu cha 130 (1) (2) (e) na kifungu cha 131 (1) cha kanuni ya adhabu kama kilivyofanyiwa malejeo mwaka 2002.
Hivyo mahakama ikamtia hatiani Victory mlowe kutumikia kifungo cha miaka 30 jera pamoja na viboko 12 na kumlipa fidia shilingi lakitano mhanga huku rufaa ikiwa wazi kwa mtuhumiwa
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.