ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 2, 2018

VIDEO:- WAZIRI LUGOLA ATOA TAMKO TUKIO LA MWANAFUNZI KUPIGWA HADI KIFO, MGAMBO WA JIJI DHIDI YA MWANANCHI DAR

GSENGOtV
Wizara wa Mambo ya Ndani ya nchi imekemea kushamiri kwa matukio ya watu kujichukulia sheria mkononi ikiwemo kupiga, kujeruhi na kuuawa.
Waziri Lugola amesema hayo leo Jumapili Septemba 2, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.
Ametaja matukio ya walimu kuwaadhibu, kujeruhi na kusababisha vifo vya wanafunzi wao pamoja na mgambo wa Jiji la Dar es Salaam kuwajeruhi wananchi wanaposimamia suala la usafi kuwa miongoni mwa matukio yasiyokubalika mbele ya macho ya sheria.

🕎....KWA UKAMILIFU BAADHI YA MATUKIO HAYO.
1. Wananchi kuwapiga watu wanaowatuhumu kwa makosa mbalimbali
-------------------------------------------------------------------
2.Walimu kuwapiga wanafunzi kinyume cha sheria.
-------------------------------------------------------------------
3.Mgambo kuwapiga wananchi kwa sababu ya tuhuma mbalimbali kama ambavyo wengi tumeshuhudia video ikionesha mgambo jijini Dar es salaam wakimpiga raia mmoja kwa kutumia gongo katima miguu yake tena eneo la mifupa.
-------------------------------------------------------------------
4.Askari Polisi kutumia nguvu isiyo ya kadri kulingana na mazingira halisi wanapowadhibiti watuhumiwa.
-------------------------------------------------------------------
5.Ugomvi wa kifamilia ndani ya ndoa ambao huhusisha Wanaume kuwapiga wake zao au Wake kuwapiga waume zao. .
-------------------------------------------------------------------
By Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mhe. Kangi Lugola

Akiwa #Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.