ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 3, 2018

BAADA YA UKAME WA MUDA MREFU RAIS MAGUFULI ASHUSHA NEEMA KWA WAFANYAKAZI BANDARI YA MWANZA



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Rais Dk. John Magufuli ameahidi kulipa madeni ya mishahara ya wafanyakazi wa 'Marine Service' jijini Mwanza ambao wanadai shilingi bilioni 3.7 na atawalipa ndani ya wiki huku akiwaonya kufanya kazi kwa juhudi na  ipasavyo.

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo  leo akiwa jijini Mwanza kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Meli mpya na Chelezo katika Ziwa Victoria, ambapo  ujenzi huo utagharimu shilingi Bilioni 88. 76.

''Mimi nitawapa hizo bilioni 3.7 ndani ya wiki mbili, sasa ole wenu msifanyekazi tena mtazitapika, nawaambia kabisa huu sio muda wa kubembelezana lazima tubanane kwa sababu tumechelewa'', ameonya Rais Magufuli.

Wafanyakazi hao wanadai malimbikizo ya mishahara ya takribani miezi 27 ambapo  Rais Magufuli ameeleza kuridhishwa na mwenendo wa uendeshaji wa sasa wa Marine Service chini ya Kaimu Mkurugenzi Erick Hamis.



"Kwa kazi nzuri waliyoifanya wafanyakazi wa Bandari ya Mwanza. Mhe. Rais John Pombe Magufuli ameahidi ndani ya wiki 2 kuwalipa mishahara yao yote iliyolimbikizwa kiasi cha shilingi bilioni 3.7" 

"Watanzania ni wajanja mradi ni wao lakini unaweza kushangaa wakawa wanaiba mafuta,  lakini tutabana kiasi kwamba ukiiba hata msumali utautapika..nataka value for money ionekane,  South Korea ninaimani nao. Ni watu waliokomited kufanya kazi...wapo tayari kujitolea ndiyo maana kwenye historia ilifika mahali walijitolea kunyoa nywele zao kuuza ili wapate mitaji na leo wako hapa."

 "Ninawahakikishia watanzania fedha zenu mnazozikusanya hazitopotea."

"Tusikwepe kodi ukilipa kodi fuatili Hakuna taifa litalipa kodi kisha watuletee sisi,  Tumechelewa ndugu zangu watanzania Hatukutakiwa kuwa masikini hivi." 

Kisha JPM akarudia kunukuu aneno yake anayopenda kuyatumia mara kadhaa "Hii nchi ilipaswa kuwa nchi kati ya wafadhili"

"Tujiulize kwanini ATCL ilitafunwa mpaka ikamaliza meli zote,   TTCL ambayo ilikuwa dhoofu hata leo ndiyo imeanza kuinuka mpaka inazalisha faida...Kwanini viwanda vya Tanzania vilikufa ile hali waliokuwa wakiongoza ni Watanzania. Kwanini TANALEC haipo yamebaki magofu pale...Haya ndiyo maswali ya msingi ya kujiuliza"

Rais yupo ziarani katika mikoa mitatu ya Mwanza, Simiyu na Mara ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.






















Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.