Breaking news saa kadhaa zilizopita Kivuko cha MV Nyerere kinachotoa huduma ya usafiri majini ndani ya Ziwa Victoria kati ya Bugolola Kisiwa kikubwa na Bwisha Kisiwa cha Ukara kinazama kikiwa na abiria (idadi haijajulikana bado) hivyo jitiada zinaendelea kuokoa abiria waliokuwemo.
Tayari mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella tayari kafika eneo la tukio, zaidi waandishi wetu wako eneo la tukio na habari kamili kuwajia hivi punde.
Kwa Updates zaidi Sikiliza @jembefm #JembeHabari
@gsengotv
MUENDELEZO.
KIVUKO cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza kimezama ziwa Victoria.
Inadaiwa kwamba kivuko hicho kimezama kikiwa na abiria ambapo hata hivyo bado haijafahamika idadi ya abiria waliokuwemo ingawa taarifa za awali zinadai kilikuwa na abiria zaidi ya 90.
Kwa mujibu wa baadhi ya waliozungumzia kivuko hicho wamedai kilikuwa kinatokea Bugorora kwenda Ukara kati ya saa 6 na saa 7.30 mchana na kilizama dakika kama 5 kabla ya kufika kwenye ghati ya Ukara.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamedai kuwa ghafla kilianza kutitia kwenye maji kwa nyuma kulikokuwa na mzigo na kuwezesha abiria waliokuwa mbele kurukia majini na kuogelea na mitumbwi iliyokuwa pale kufanya kazi ya kuwaokoa abiria waliorukia majini.
Pia inadaiwa abiria wengi waliokuwa ndani ya Mv Nyerere hawakuweza kutoka na kuwa wamezama.
Mmoja ya waliozungumzia kuzama kwa kivuko hicho amedai idadi ya abiria waliopanda haijulikani ingawa uwezo wa kivuko ni kubeba abiria 150.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo hazikufanikiwa kwani simu yake haikuwa hewani.
Hivyo tutaendelea kuwajuza kinachoendelea na idadi kamili au abiria waliokuwamo kwenye kivuko hicho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.