ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 24, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
 




TELEGRAMS:   POLISI,                                                                                                     OFISI YA
TELEPHONE: 2500712                                                                                  KAMANDA WA POLISI,
Fax: 2502310                                                                                                 MKOA WA MWANZA,
E-mail: mwapol@yahoo.com                                                                                        S.L.P. 120,
           rpc.mwanza@tpf.go.tz                                                                                MWANZA.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 23.08.2018


¨       MAGARI MAWILI YANAYOBEBA WANAFUNZI YAMEGONGANA NA KUSABABISHA KIFO KWA MTU MMOJA NA KUJERUHI WATU KUMI WILAYANI ILEMELA.

KWAMBA TAREHE 23.08.2018 MAJIRA YA SAA 05:50HRS ALFAJIRI KATIKA BARABARA YA MWANZA KWENDA SIMIYU ENEO LA NANENANE WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T.506 BYE AINA YA MITSUBISHI ROSA, MALI YA SHULE YA KIVULINI PRIMARY SCHOOL, LIKIENDESHWA NA DAEREVA AITWAYE KURWA CHARLES @ WAYALA MIAKA 27, MKAZI WA KISESA, LILIGONGANA NA GARI NAMBA T.745 ANF AINA YA NISSANI CIVILIAN, MALI YA NYAMUGE PRIMARY SCHOOL, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE ALBERT MUSA @ JORAM, MIAKA 58, MKAZI WA NYAMUGE NA KUSABABISHA KIFO KWA DEREVA WA GARI LA NYAMUGE PRIMARY SCHOOL  ALBERT MUSA @ JORAM KISHA KUJERUHI WANAFUNZI NANE, DEREVA WA GARI LA KIVULINI  PAMOJA NA KONDAKTA WA GARI LA NYAMUGE.

WANAFUNZI WATATU MAJERUHI PAMOJA NA DEREVA WA GARI LA KIVULINI PRIMARY SCHOOL WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, VILEVILE KONDAKTA WA GARI LA NYAMUGE PRIMARY SCHOOL BWANA ISAYA JOSEPH, MIAKA 21, AMELAZWA HOSPITALI YA SEKOU TOURE AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, HALI ZAO WOTE ZINAENDELEA VIZURI.  AIDHA WANAFUNZI WATANO TAYARI WAMEPATA MATIBABU KATIKA ZAHANATI YA BUZURUGA HALI ZAO NI NZURI NA TAYARI WAMERUHUSIWA.

AIDHA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA CHANZO CHA AJALI NI UZEMBE WA DERE WA GARI LA KIVULINI AMBAYE ALIHAMA UPANDE WAKE KISHA KWENDA KULIGONGA  GARI LA SHULE YA MSINGI NYAMUGE. POLISI BADO WANAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA AJALI HIYO, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA NA KUBAINI UPO UZEMBE BASI DEREVA WA GARI LA KIVULINI ATAFIKISHWA MAHAKAMANI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI  WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO AKIWATAKA KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI NA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA. SAMBAMBA NA HILO PIA ANAWATAKA WANANCHI WAPAZE SAUTI DHIDI YA MADEREVA WAZEMBE ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUSHUGHULIKIWA KWA MUJIBU WA SHERIA.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.