Kocha Msaidizi wa klabu ya Simba, Masoud Djuma muda wowote kuanzia sasa ataachana na klabu ya Simba baada ya Klabu ya Simba Kufikia makubaliano kuvunja mkataba.
Taarifa za ndani kutoka bodi ya wakurungezi wa klabu hiyo wamefikia uamuzi huo wa kumuondoa kutokana na kutengeneza mgogoro kati ya wachezaji na kocha mkuu wa klabu hiyo kwa kuwaambia wachezaji kucheza chini ya kiwango ili kocha mkuu afukuzwe na yeye awe kocha mkuu wa klabu hiyo.
Pia Masoud anatajwa kuwa hana maelewanao mazuri na kocha mkuu wa klabu hiyo Patrick Aussems na sasa ni mara ya pili kwa kocha huyo kutoelewana na makocha wakuu wa klabu hiyo kwani hata Pierre Lenchatre alishindwa kuongezewa mkataba mpya sababu mojawapo ni kutokuwa na maelewano mazuri na Masoud Djuma.
Inaelezwa kuwa leo au kesho klabu ya Simba inaweza kutoa taarifa kwa vyombo vya habari ya kusitisha mkataba wa kocha Masoud Djuma ambaye amekuwa kipenzi kwa wanachama na mashabiki wa klabu hiyo Kutokana na sababu hizo mbili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.