ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 19, 2018

MBUNGE SHANIF MANSOOR AWALIPIA BIMA ZA AFYA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI JIMBO LA KWIMBA.NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGO TV
Mbunge wa jimbo la kwimba Mkoani Mwanza SHANIF MANSOOR, mbunge wa vitendo katika ziara yake ya siku sita jimboni kwake akitembelea  miradi ya maendeleo amewakabidhi wajumbe Halmashauri kuu CCM na kata, matawi, CCM wilaya ya kwimba, BIMA za Afya zaidi ya mia tatu sabini.

MANSOOR, amewahakikishia watendaji wote kutoka wilayani kwake kuwa wananufaika na chama cha mapinduzi CCM kwa kuwalipia bima za Afya kutokana na mchango wao mkubwa kwenye maendeleo ya jimbo.

AGNES BASHEMU, katibu wa (UWT) mkoa wa Mwanza amempongeza MANSOOR, kwa jitihada zake za dhati katika kuwahudumia wananchi wa jimbo hilo na kushiriki katika kuwatatulia changamoto zao sugu zilizokuwa zikiwasulubu kwa muda mrefu sasa, hususani kero ya maji, umeme, afya, kilimo na elimu.

Kwenye ziara hiyo ya Mhe. Mansoor, akiwa ameambatana na MH.MTEMI MSAFIRI, mkuu wa wilaya ya kwimba mkoani Mwanza pia aliweza kutembelea majengo matano ya kituo cha Afya Malya mjini, kilichojengwa kwa fedha za serikali kiasi cha shilingi Milioni mia nne.

"Pamoja na ukarabati wa majengo ya zamani, ujenzi huo umefikia hatu za mwisho wakati fedha bado ipo" alisema MTEMI MSAFIRI.


SHANIF MANSOOR, akioneshwa kufurahishwa na utendaji wa mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa Serikali tayari imetoa fedha kiasi cha shilingi milioni mia nne tayari kwaajili ya ujenzi wa kituo kipya kikubwa cha Afya cha Mwamashimba.Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.