ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 16, 2018

MAHAKAMA YAAHIRISHA KESI YA WEMA SEPETU.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam leo ilitarajiwa kutoa hukumu juu ya kesi inayomkabili muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu na hukumu hiyo kuahairishwa hadi siku ya ijumaa tarehe ishirini mwezi kutokana na hakimu anae simamia kesi ya msanii huyo kuhitaji muda wa kufanyia uchunguzi baadhi ya mambo ili atoe huku iliyo sahihi bila kuelemea upande wowote.

ambapo kwa upande wake wema sepetu amedai kuwa anasubir maamuzi ya mahakama itakaloamua kwani kwa upande wao wa utetezi wameshamaliza kujitetea hivyo wanasubiri mahakama itoa maamuzi kama ni kukutwa n hatia au la.

Nikujuze tu kuwa msanii wema sepetu anakabiliwa na kesi ya kukutwa na msokoto wa bangi pamoja na karatasi maalum za kuvutia dawa hizo baada ya jeshi la polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake.

Mbali na Wema washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.