CHANZO/MWANANCHI
Dar es Salaam. Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo amesema rehema za Mungu ndizo zimefanya ateuliwe kushika wadhifa huo.
Dar es Salaam. Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo amesema rehema za Mungu ndizo zimefanya ateuliwe kushika wadhifa huo.
Jokate ni miongoni mwa walioteuliwa jana Julai 28, 2018 na Rais John Magufuli katika mabadiliko ya viongozi kwa baadhi ya maeneo wakiwamo wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na makatibu tawala.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Jokate amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini.
“Unaweza ukawa unapitia mitihani migumu sana kwenye maisha yako, lakini inakubidi usikate tamaa kwa sababu tu ya wale wanaokutegemea, wanaokuangalia na kuvutiwa nawe na kujifunza kupitia maisha yako.”
“Lakini zaidi kwa sababu safari ya mafanikio ina milima na mabonde, inabidi upambane na kiukweli hakuna mafanikio yasiyokuwa na changamoto. Na kuna muda changamoto ndiyo hasa zinatengeneza character zetu,” ameandika Jokate.
“Kikubwa zaidi wakati wa changamoto tukumbuke kuwa wanyenyekevu, wenye kujishusha na kumuomba Mungu aendelee kutupa imani, hekima na busara ya kusubiri wakati wake. Tukumbuke Mungu hamtupi mja wake,” ameandika Jokate aliyeshika nafasi ya pili katika shindano la mlimbwende wa Tanzania (Miss Tanzania) mwaka 2006.
Miezi kadhaa iliyopita Jokate aliondolewa kwenye nafasi ya kaimu katibu wa idara ya uhamasishaji na Chipukizi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.