GSENGOtV/ZEPHANIA MANDIA
Wakati Serikali ikihaha kuhakikisha kuwa inawahudumia wananchi wake kwa kusaka fedha za kugharimia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ile ya afya, Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor amewataka watendaji wa Halmashauri yake kuhakikisha kuwa wanasimamia vyema fedha zilizotolewa na Serikali kwaajili ya ujenzi wa kituo kikubwa cha kisasa cha Afya kitakacho vihudumia vijiji vyote jirani wilayani humo hata kupunguza msongamano kwenye hospitali za wilaya jirani ikiwemo Mwanza mjini (Nyamagana)
Mansoor ameyasema hayo mwishoni mwa wiki katika kata ya Mwamashimba wilayani Kwimba, wakati akitoa maagizo katika mkutano alioketi na wananchi pamoja na viongozi watendaji jimboni kwake kujadili harakati za kuanza rasmi kwa ujenzi wa Kituo cha Afya.
"Huu ni mradi wetu nawasihi wote mnaopaswa kusimamia muwe waadilifu, mjitolee ili mradi ukamilike kwa ubora, viwango na kwa wakati, tumepewa miezi mitatu hivyo kufikia Novemba 30 mradi uwe umekamilika" alisema Mansoor.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mtemi Msafiri amesema kuwa maendeleo hayo yanajengwa kwa manufaa ya wananchi wote pasipo kubagua vyama wananchi hawanabudi kushirikiana na Serikali ili kuifikisha nchi kwenye adhma yake ya Uchumi wa Kati.
"Kama ninavyowaona wengi hapa mmevaa tisheti zenye ujumbe 'HAPA KAZI TU' Mhe. Magufuli wakati anakabidhiwa urais hiyo ndiyo Kauli mbiu yake iliyombeba, na sisi Kwimba tukaitafsiri 'KWIMBA KAZI NA MAENDELEO'." na kuongeza
"Mhe mbunge wetu amepigana kweli bungeni kuhakikisha kuwa fedha zinakuja na sasa tunajivunia kuwa na eneo la hospitali lakutosha, tutatengeneza wodi kubwa ya kisasa, vyumba vya kisasa kwa akinamama kujifungulia na huduma nyingine zote za afya ngazi ya kiwango cha kati, hili litasaidia kutuepusha na vifo vinavyoweza kuzuilika na pia lile suala la kuwa tegemezi kwa hospitali za wilaya nyingine kubwa kama Nyamagana na Ilemela"
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.