ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 12, 2018

BILIONI 2.3 KUTUMIKA UJENZI WA KIVUKO KISIWA CHA BEZI.



Na James Timber, Mwanza

Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko katika kisiwa cha Bezi kilichopo Kata ya Kayenze wilayani Ilemela Mkoa wa Mwanza

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela jijini hapa Angeline Mabula katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi jimboni kwake, amesema kuwa katika kuboresha huduma za usafiri kisiwani hapo ambapo zabuni imechukuliwa na Sangoro Marine kwa ajili ya kutengeneza kivuko hicho.

Mbunge Mabula amesema fedha hizo zimekabidhiwa TEMESA, kwa muda wowote wataanza ujenzi wa kivuko ili kuboresha huduma ya usafiri katika kisiwa hicho.

"Hiyo ni ahadi yangu niliyoitoa mbele ya wananchi kuwaboreshea huduma ya mawasiliano na huduma ya usafiri naamini litafanyiwa kazi muda wowote kinachosubiriwa ni maombi yao ya  msamaha wa kodi kwa Sangoro Marine ili aanze ujenzi huo haraka," alisema.

Pia amesema kuwa alipeleka wataalamu wa mawasiliano kwa ajili ya kukagua eneo ambalo litawekwa mnara kwa lengo la kuboresha huduma ya mawasiliano katika kisiwa cha Bezi na Kituo cha Afya cha Sangabuye ambapo waliahidi kujenga mnara huo haraka.

Kwa upande wake Mkazi mmoja wa Kisiwa cha Bezi Sophia Charles ameeleza kuwa kutokuwa mawasiliano  na huduma bora ya usafiri katika kisiwani hapo kumesababisha baadhi ya wakina mama wajawazito kutokufika Kituo cha Afya cha Sangabuye mapema ajili ya kupata huduma ya uzazi.

Aidha Sophia ameshukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwakumbuka kwani baadhi yao walikuwa wanazalia njiani kutokana na kutokuepo kwa huduma bora za mawasiliano na usafiri, na kubainisha kuwa kupata gari la wagonjwa ni mawasiliano na gari hilo haliwezi kuja kufuata mgonjwa kisiwani hapo wakati hamna huduma ya kivuko.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.