ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 1, 2018

AJALI MBAYA YA MAGARI MANNE YASABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI.

MBEYA. Watu 20 wamekufa papo hapo na wengine 45 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea Mlima Iwambi wilayani Mbeya.
Ajali hiyo iliyotokea leo Julai Mosi, 2018 imehusisha magari manne zikiwamo daladala tatu na lori moja.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu ametoa taarifa hiyo baada ya kazi ya uokoaji kukamilika.
Wananchi wakishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama walishiriki katika uokoaji. Moja kati ya daladala hizo lililaliwa na lori.
Lori liliyagonga magari hayo yaliyokuwa yakitokea stendi ya Mbalizi kuelekea Mbeya mjini.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alikuwapo eneo la tukio ambako kazi ya uokoaji ilishirikisha vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.