ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 10, 2018

WAZIRI MKUU AANDAA FUTARI KWA VIONGOZI MKOANI MWANZA.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini zote kutokubali kugombanishwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema taifa na badala yake waendelee kushirikiana ili kuimarisha amani nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa rai hiyo jana wakati akizungumza kwenye hafla ya futari aliyoiandaa kwa viongozi wa viongozi na waumini wa dini za Kiislamu, Kikiristo na serikali iliyofanyika katika viunga vya Chuo cha Benki Kuu, Capripoint Jijini Mwanza.

Mhe.Majaliwa aliwahimiza viongozi wa dini zote kufanya kazi kwa misingi iliyowekwa na kwamba inapotokea jambo lolote haliko sawa walitatue kwa njia ya mazungumzo akisema serikali iko tayari kuendelea kushirikiana na dini zote.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Mwanza, Askofu Charles Sekelwa alisema viongozi wa dini wataendelea kushirikiana na serikali kuimarisha umoja na mshikamano uliopo, akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella kwa ushirikiano wake wa dhati.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.