ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 14, 2018

SERIKALI YASIKIA KILIA CHA KUPUNGUZA KODI TAULO ZA KIKE.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ametangaza rasmi kupendekeza kuondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye taulo za kike nchini ili kuweza kuwapa fursa wanafunzi waliopo mashuleni na vijijini kuzipata kwa bei nafuu.

Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo leo Juni 14, 2018 wakati alipokuwa anaendelea kusoma bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19 na kusema amefanya uamuzi huo kutokana na sheria ya kodi ya ongezeko la thamani kumpa mamlaka ya kufanya hivyo.

"Napendekeza kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye taulo za kike, lengo la hatua hii ni kuwezesha upatikanaji wa bidhaa hiyo adimu kwa bei nafuu ili kuweza kulinda afya ya mama na mtoto wa kike hasa watoto waliopo mashuleni na vijijini", amesema Dkt. Mpango.

Pamoja na hayo, Dkt. Mpango ameendelea kwa kusema "ni matarajio ya serikali watengenezaji wa bidhaa wa taulo za kike wataziuza kwa bei nafuu baada ya kusamehewa kodi hii hatua".

Mbali na serikali ya awamu ya tano kuona umuhimu wa mtoto wa kike katika suala taulo za kike ,Kampuni ya East Africa Television LTD imefanya kampeni ya Namthamini kwa miaka miwili mfululizo ikiwa na lengo la kumsaidia mtoto wa kike kupata pedi kwa urahisi, ambapo imezunguka shule mbalimbali nchini Tanzania na kugawa taulo hizo baada ya wananchi  mbalimbali kujitokeza kuchangia.  Jumla ya mabinti 673 waliweza kufikiwa na kampeni ya Namthamini kwa mwaka 2017, na kwa mwaka 2018 kampeni hii ilifanikiwa kufikia zaidi ya mabinti 1500 Tanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.