NA ZEPHANIA MANDIA G.SENGOtV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imemhukumu mshtakiwa Daudi Magesa ambaye ni fundi simu kifungo cha mwaka mmoja nje bila kutenda kosa lolote pamoja na kutaifisha na kuharibu vifaa alivyokuwa akivitumia baada ya kumkuta na hatia ya kutenda kosa la kughushi namba tambulishi za simu (IMEI) kinyume na kifungu namba 154 na 135/158 ya sheria ya mtandao na mawasiliano ya posta namba tatu ya mwaka 2010.
Akitoa hukumu hiyo hii leo, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bahati Chitepo, amesema mahakama imemkuta na hatia ya makosa yote, mshtakiwa mwenyewe kakiri kutenda kosa hilo na vielelezo vyote vilivyowasilishwa vinathibitisha kutenda kosa hilo.
Johaness Kalungura, Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA , amesema Watu hawa ni hatari wanatumia software na kubadilisha IMEI mtu ambaye ni mhalifu anaendelea kutenda uhalifu na asiyemhalifu simu yake inabadilishwa, wakati vyombo vya dola vinamtafuta mhalifu vinashindwa kuwatambua na kusababisha kukamatwa kwa mtu asiyehusika na mhalifu anaachwa,” alisema Kalungura.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.